Profile cover photo
Profile photo
Mohamedi Mtoi
376 followers
376 followers
About
Posts

Add a comment...

TAFAKURI CHOKONOZI: POLISI, MBONA KWINGINE HAMKOMAI KAMA HUKU?!

Ulinzi tulio upata leo wa kuzungukwa na gari za Polisi na Polisi wenye Mbwa na Mabomu tukiwa ofisini (Makao makuu) ili tu kuzuia maandamano ya amani ambayo mwisho wake yalifanywa na kundi lingine na ofisi za mkoa wa Ilala kufungwa siku nzima ya leo ni ushahidi tosha kuwa kuuwawa na kunyofolewa viungo kwa ndugu zetu Albino ni kwa kuwa serikali haija amua kuwalinda kwa dhati kama wanavyokomaa na CHADEMA ili wasiandamane.

Ulinzi wa leo umedhihirisha kuwa CCM wako radhii iwawatumie Polisi kuithibiti CHADEMA wasiandamane lakini wanyama kama Twiga na Tembo ambao ni wakubwa kuliko mwili na uzito wa binadamu waachwe wakiibwa kwenda Arabuni huku Polisi yenye silaha kama za leo ikiwa kimya na wao wakiwa bar wakigongea mivinyo na mapaja ya kuku.

Mkwara na mbwembwe zilizo onyeshwa leo na jeshi la Polisi na bado maandamano yakafanywa ina onyesha ni namna gani Polisi na serikali yake wana waogopa CHADEMA kuliko mafisadi ambao JK aliwapigia magoti warudishe hela ya EPA bila kuwakamata na bila kutumia nguvu kama walizo tumia kwetu leo. Kumbuka kuna wizi wa Escrow akaunti mkubwa kuliko EPA na bado wezi hawaja kamatwa na jeshi hilihili lenye mikwara na silaha hizihizi lipo!

Nguvu na mbwembwe zinazo onyeshwa na Polisi kwetu (CHADEMA) kama zingetumika kuwakamata wale wauza unga ambao JK alisema ana wajua na majina yao anayo; basi leo hii kusinge kuwa na kundi la vijana wanao geuka kuwa mazezete kwa kutumia unga na wengine kufanywa Punda wabeba unga kuwanufaisha wajanja wachache.

kama hizi nguvu hizi zinazo tumiwa na Polisi kwa maagizo ya wale jamaa zao zingetumika kuwakamata Mafisadi wafuja mali ya umma na kusimamia maadili ya Taifa naamini hata kile wanacho kitetea pale Dodoma ili tusiandamane kukipinga kisinge kuwepo kwenye mjadala na tungeokoa fedha nyingi ambazo zingeenda kufanya mambo mengine ya manufaa kwa taifa hili.

Pamoja na kuwatumia sana Polisi, Naamini hata hao Polisi wanapenda vizazi vya taifa hili na ndugu zao wapate katiba bora, maisha bora na huduma bora, Naamini Polisi wanatumiwa sio kulinda maslahi mapana ya nchi bali maslahi ya watu wachache walio amua kuziba masikio ili wasisikie sauti za wananchi, Naamini hawata watumia Polisi kuomba kura!

Naamini wanajua katiba mpya haita patikana kwa namna wanavyo taka wao, kwa matakwa yao, na kwa mabavu yao na kwa nguvu zao za kutumia Polisi. Naamini wanajua kuwa wamepotoka ila nafsi zao hazitaki kukubali maana kwao la muhimu ni yale mafurushi ya fedha.

Mungu wetu wa haki amewaona na atalinda kucha na meno yangu...
Add a comment...

UHUNI WA CCM KATIBA MPYA WAZIDI KUKATALIWA.

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi

MAKAMU wa Rais Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amesema maoni yaliyotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) juu ya Bunge Maalumu la Katiba, hayajatekelezwa na hivyo watapita kwa Watanzania na waumini wao kuwaeleza nini cha kufanya.
Jukwaa hilo lilikutana Agosti 27 hadi 28, mwaka huu na kujadili hatima ya Bunge hilo na kutoa mapendekezo sita, moja ikiwa ni kusitishwa kwake.
Akizungumza na gazeti hili jana, Niwemugizi ambaye pia ni mjumbe wa TCF, alisema:
“Tunaona Bunge bado linaendelea na Serikali iliyopo madarakani inaendelea na mipango yake, haiheshimu wala haitekelezi ushauri unaotolewa.

“Sauti nyingi haziridhiki na yale yanayotendwa na Bunge Maalumu la Katiba, hawajui ni kiasi gani Watanzania wameshapevuka na wanatambua haki zao.”
Alisema wamejipanga kurudi kwa Watanzania kuwafahamisha na kuwafundisha ili watambue haki na wajibu wao hali itakayowasaidia kujua njia sahihi ya kufanya.
“Wanaweza kutudharau kwamba sisi hatuna chochote, kwakuwa hawajali tuliyopendekeza, tutarudi kwa watu wetu tunaowaongoza, kitakachotokea hatujui.

“Sisi tunaamini kurudi kwa Watanzania ni sehemu pia ya injili kwa sababu kuna injili ya jamii, na tutawafundisha watambue haki na wajibu wao na namna sahihi ya kufanya,” alisema.
Askofu huyo alisema wanachotaka Watanzania ni kuona mambo yakienda vizuri, hivyo kama viongozi wanakataa ushauri unaotolewa, Watanzania wataamua cha kufanya.

Kuhusu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, askofu huyo alisema amejidhalilisha kwa kauli zake za kejeli ndani ya Bunge hilo.
“Mkishakuwa na viongozi wenye dharau na kejeli, hapo nchi imekwisha kabisa. Sitta amejidhalilisha kwa kauli zake, hasa ukizingatia kuwa na yeye anatajwa kutaka kugombea urais, sifa zake zinazidi kupungua,” alisema.

Jukwaa hilo linaundwa na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Jumuiya ya Kikristo (CCT) na Makanisa ya Kisabato (SDA).
Tamko la jukwaa hilo lililotolewa Agosti 28, mwaka huu, lilisema mjadala wa Bunge hilo umeondoa maoni yaliyotolewa na wananchi kuhusu muundo wa Muungano, kupunguza mamlaka ya Rais, uwajibikaji na uwajibishwaji wa wabunge na ukomo wao.
“Wamewezesha maoni na maslahi ya chama tawala kwa uongozi wa kikundi cha wanasiasa wachache wasio na uaminifu na uadilifu wa kutosha kuwekwa kama mapendekezo ya Katiba mpya kwa nia ya kulinda maslahi binafsi au ya makundi na kuhalalisha ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na maadili ya uongozi bora,” inasema sehemu ya tamko hilo.

Kutokana na hali hiyo, jukwaa hilo lilitoa mapendekezo sita likitaka yafanyiwe kazi.

MAPENDEKEZO YA JUKWAA
1. Serikali (Wizara ya Katiba na Sheria) irudishe tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na nyaraka zake zote kwa ajili ya wananchi kuendelea kuona kazi waliyoifanya, kujifunza na kujadili Rasimu ya Katiba kwa uwazi.

2. Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea lijadili na kuboresha tu maoni yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na sio kufanya mabadiliko katika Katiba ya mwaka 1977.

3. Mchakato wa Katiba usimamishwe ili kupisha majadiliano, maelewano na maridhiano mwafaka, Uchaguzi Mkuu na wa Serikali za Mitaa. Na mabadiliko ya Katiba ya 15 ya mwaka 1977 yafanyike kuwezesha chaguzi kufanyika kwa uwazi na haki. Pia, kuweka kifungu kitakacholinda rasimu ya pili na kumtaka kiongozi ajaye kuendelea na mchakato wa Katiba.

4. Baada ya Bunge Maalumu la Katiba kuanza shughuli zake tena, Mwenyekiti wa Bunge hilo afanye kazi kwa mujibu wa kanuni na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba badala ya kutumia ubabe na kiburi cha wingi wa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi katika Bunge la Katiba.

5. Wananchi waendelee kusoma na kujadili maoni yaliyoko katika rasimu ya pili ya Katiba, na kufuatilia kitakachokuwa kinajadiliwa kwenye Bunge la Katiba ili kuwawezesha kupiga kura ya maoni wakiwa na uelewa wa kutosha kabisa kuhusu ni nini kipo kwenye “Katiba inayopendekezwa”. Wananchi pia wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa nia ya kuwawezesha kupiga kura ya maoni.

6. Tume ya Mabadiliko ya Katiba ihuishwe na kupewa mamlaka kisheria ili kuiwezesha kujibu maswali yanayojitokeza na kutoa ufafanuzi kwa Bunge Maalumu la Katiba na wananchi kwa jumla hadi Katiba mpya itakapokamilika na kukabidhiwa rasmi.
Tamko lilisema: “Jukwaa la Wakristo Tanzania na Watanzania wote wanaoitakia nchi yao mema, tunakuomba Mheshimiwa Rais kwamba AMANI ya nchi yetu sasa imo mikononi mwako, hasa katika kipindi hiki cha kuandikwa kwa Katiba mpya.
“Tunakuomba uahirishe mchakato unaoendelea ili uepushe ishara za aina mbalimbali za kuanzisha sintofahamu nchini mwetu na hali yoyote inayoweza kuathiri vibaya mshikamano, umoja na amani ya taifa letu.

“Ifahamike kuwa Wananchi wa Tanzania wako juu ya Wajumbe wa Chama cha Mapinduzi. Kwa mantiki hiyo, tunakuomba uepushe wananchi wa Tanzania kuhamasishwa kukikataa Chama cha Mapinduzi kwa kuwa tu chama hicho kimeyapuuza na kimekataa maoni yao waliyotoa kwa dhati baada ya kuaswa na kuhimizwa kufanya hivyo na viongozi wa nchi.
“Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wafanye yasiyowapasa.

“Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutabakari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao. (Rejea Warumi 1: 28-32)
“Ikumbukwe kuwa Rasimu ya Pili ya Katiba ni waraka halali na rasmi na ndiyo mawazo ya Watanzania na tunahimiza kuwa Katiba ni ya wananchi na inahitaji maridhiano na siyo ubabe.”
Add a comment...

CHADEMA UK TUNATOA PONGEZI KWA MAFANIKIO YA MKUTANO MKUU

Siku kadhaa zilizopita CHADEMA kikiwa ni chama kinachobeba ndoto za ukombozi za waTanzania walio wengi, kilipiga hatua kubwa na kukamilisha jambo la kihistoria. Baada ya kujenga chama kwenye ngazi na mashina, misingi, wilaya na kanda, CHADEMA ilifanya mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wakuu wa chama kuanzia kiti cha Mwenyeki na Katibu pamoja na mabaraza ya chama.
Katika uchaguzi huo ambao uliendeshwa kitaalamu na kwa umakini mkubwa viongozi wakuu walipatikana kwa njia ya demokrasia. Hili lilikuwa ni jambo la kishujaa lililowahakikishia wale wenye duku duku kuhusu uimara wa vyama vya upinzani kama CHADEMA ukichukulia maanani namna ambavyo serikali inatumia njia za kiharamu kuviua vyama hivi either kwa kupandikiza puppets au kwa kutumia vyombo vya dola kama Policcm kuvikandamiza. Ukomavu huu wa kisiasa ni ishara kubwa kwamba sasa CHADEMA iko tayari kuishika dola na kuwabadili waTanzania na kuwapa tena heshima yao waliyokuwa wameipoteza kutokana na mlolongo wa viongozi na serikali nyepesi zilizokosa uchungu na uzalendo kupelekea kuuza nchi na kuwaacha waTanzania wakiteseka.

Sisi CHADEMA UK tunapenda kuchukua nafasi hii kuipongeza safu nzima ya ungozi kwa kupata dhamana ya kukiongoza chama. Kipekee na makusudi ya dhati kabisa, tunapenda kumpongeza kamanda Mbowe na Dr Slaa kwa kukubali tena kuipeperusha bendera ya chama wakati huu muhimu tunapoelekea uchaguzi mkuu 2015. Tunapenda kusema kwamba, imani yetu kwa viongozi hawa ni kubwa kwani ni mengi ambayo chama kimepitia chini ya safu hii imara isiyotetereka.

Tunapenda pia kuwapongeza viongozi wote wa mabaraza ya chama (BAVICHA, BAWACHA na Baraza la Wazee la CHADEMA). Mabaraza haya ambayo ni muhimili imara wa chama, ni imani yetu kwamba yamepata viongozi shupavu watakaoleta mabadiliko dhabiti na halisi ili kupambana kumtoa ccm madarakani.
Salamu zetu pia ni kwa viongozi wa ngazi mbali mbali wa chama waliochaguliwa katika hatua mbalimbali zilizokuwa na lengo la kukiimarisha chama kwenye ngazi ya msingi. Tuna Imani kwa kila mmoja yuko tayari kwa mapambano haya.
Mwisho kwa kuyatumia maneno ya Henri Ford aliyesema, “Coming together is a beginning; keeping together is a progress; and working together is a success” tunapenda kuwahakikishia kwamba CHADEMA UK itaendelea kusapoti na kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi wote wa ngazi zote za chama kwenye harakati tulizoko sasa hivi. Sisi tunaamini kwamba kwa pamoja tutaweza. Tunaamini katika kufanya kazi kama timu moja tukiwa na lengo na madhumuni mamoja. Kwa kushirkiana kama timu (TEAM: Together Everyone Achieve More) hakuna mbalo CHADEMA itashindwa kutimiza.
Mungu ibariki CHADEMA na nchi yetu ya Tanzania.

Ofisi ya katibu - CHADEMA UK
Add a comment...

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAMKO LA CHAMA JUU YA UTEKELEZAJI WA AZIMIO LA MKUTANO MKUU KUHUSU MIGOMO NA MAANDAMANO YA AMANI NCHI NZIMA

Ndugu waandishi wa habari

Tunapenda kuanza mkutano huu kwa kutoa salaam za amani kwa Watanzania wote, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Amani Kimataifa, ambayo huadhimiswa Septemba 21, ya kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu kama ilivyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ni ‘The Right Of People’s to Peace’.

Tumekutana nanyi hapa siku hii mahsusi ya kuazimisha amani kimataifa, tukiwa na ujumbe maalum kwa Watanzania kuwaeleza namna ambavyo watawala wa Serikali ya CCM, wanavyohatarisha amani ya nchi yetu kwa kuvunja haki za msingi za Watanzania huku pia wakififisha matumaini ya wananchi.

Tunataja maneno hayo mawili HAKI na MATUMAINI kwa makusudi kabisa kwa sababu hayo ndiyo ndiyo msingi wa amani na utulivu wa kweli mahali katika taifa ambalo linajali na kuzingatia maendeleo na ustawi wa wananchi wake.

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake kali kuonesha namna ambavyo walioko madarakani wanahatarisha amani na utulivu wan chi, aliwahi kusema kuwa ni hatari sana iwapo wananchi wakipoteza matumaini kwa viongozi wao huku pia hawaoni haki ikitendeka. Mwalimu alikwenda mbali na kusema Watanzania watakuwa ‘wapumbavu’ wakikubali viongozi waendelee kwenda kinyume na maslahi au matakwa ya wananchi wao.

Kama wananchi hawapati haki na wanapoteza matumaini na viongozi wao, hakuwezi kuwa na amani na utulivu. Itabaki amani inayoimbwa na CCM majukwaani wakati haki za msingi ndani ya nchi zikiminywa na kukiukwa.

Ni vigumu kuwa na amani au utulivu wa dhati iwapo haki za kisiasa (mf; kukutana, kuandamana n.k), haki za kiuchumi (kuwa na maisha bora) haki za kijamii (kupata elimu bora na bure, matibabu bora na bure, maji safi na salama), n,k, huku ufisadi na ubadhirifu wa mali na rasilimali za umma, ukiongezeka na UWAJIBIKAJI ukiwekwa kapuni.

Ndugu waandisi wa habari, ninyi pia ni mashahidi wa namna ambavyo utawala huu wa CCM ambao umeshapoteza kabisa ushawishi wa kisiasa kwa wananchi, umezidi kuminya haki ya kupata taarifa huku pia ikiendelea kutumia sheria za kikoloni kuminya uhuru wa habari nchini.

Hali hii imewafanya waandishi makini wanaozingatia miiko na maadili ya taaluma yao, kuwa wahanga wa vitendo viovu vya watawala, wakiwemo askari polisi kama ilivyodhihirika hivi karibuni mbele kabisa ya milango ya wakubwa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani. Ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya namna hiyo ambayo yalifikia hatua ya juu pale askari walipomuua kikatili Mwandishi Daudi Mwangosi, Septemba 2, 2012, huko Nyololo, Iringa

Tungependa pia kutumia nafasi hii Siku ya Amani Kimataifa, kuwatia moyo ninyi waandishi wa habari kuendelea kutekeleza wajibu wenu wa kijamii (social responsible journalism) kwa kuzingatia maslahi na matakwa ya wananchi, tukiungana na Watanzania wengine wanaothamini na kutambua uhuru wa habari kama moja ya mihimili muhimu katika ujenzi wa demokrasia na hatimaye maendeleo na ustawi wa wananchi wote.

CHADEMA inaungana na Watanzania wote ambao wako sambamba nanyi katika kuheshimu wajibu, majukumu na taaluma yenu, hususan katika kipindi hiki ambapo vyombo vya habari na waandishi wanaojipambanua kwa umakini wa kuwatumikia Watanzania, kama ilivyo kwa watu wengine makini kwenye makundi mbalimbali ya kijamii, wanalazimika kupitia kwenye ‘bonde la kifo’ linalotengenezwa na watawala waliopoteza uhalali na ushawishi wa kisiasa, wakikabiliwa na hofu ya anguko kubwa kutoka madarakani.

Katika siku hii ya leo, tukiunganisha na mfululizo wa matukio ya vyombo vya dola kugeuka kuwa adui wa raia na mali zao, ikiwemo kushambulia waandishi wakiwa kazini, tunao wajibu wa kuwataka watawala kutambua wajibu wa kitaaluma na uhuru wa waandishi wa habari kwa ajili ya kuweka misingi ya amani na utulivu unaotokana na haki na matumaini. CHADEMA ni moja ya wadau wa habari ambao wameweka saini kukubaliana na Azimio la Dar es Salaam Juu ya Uhuru wa Uhariri na Uwajibikaji (DEFRI), ambalo iwapo Serikali ya CCM ingekuwa imelikubali, kulithamini na kulizingatia, leo hii lingeweza kuwa moja ya nyaraka zinazotutambulisha duniani kama taifa linalotukuza haki, matumaini, uhuru na uwajibikaji kwa ajili ya wananchi.

Tumeomba kukutana nanyi leo ili tuweze kutoa kauli juu ya Siku ya Amani Kimataifa, sambamba na yanayoendelea kuhusu Azimio la Mkutano Mkuu wa Chama; kufanya maandamano na migomo ya amani nchi nzima isiyo na ukomo kupinga ufisadi unaofanywa na Bunge Maalum la Katiba, kupinga uchakachuaji wa maoni ya wananchi unaoendelea kufanyika mjini Dodoma na uvunjifu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Katika muktadha huo wa Siku ya Amani Kimataifa, tungependa kuelezea uhalali wa maandamano na migomo hiyo ya amani kama ifuatavyo;

Maandamano; Haki na Wajibu wa kikatiba;

Kwanza kabisa, Watanzania wote wanawajibika kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, Ibara ya 27 (1)-(2), ambayo inasema;

“(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine. (2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”

Azimio la Mkutano Mkuu wa Chama la kufanya maandamano na migomo ya amani nchi nzima lilizingatia takwa hili la Katiba ya Nchi. Kinachoendelea huko Dodoma ni uharibifu na ubadhirifu wa mali na rasilimali za umma. Ule ni ufisadi. Kwa sababu Katiba Mpya haitapatikana kwa namna ile bunge linavyoendelea Dodoma. Hata Rais Jakaya Kikwete amekubali hilo mbele ya viongozi wenzake. Ni wajibu wetu sote kupinga Bunge la Katiba kuendelea.

Pamoja na ubovu wake ilionao, Katiba ya Nchi, katika Ibara ya 20 (1), imetoa haki kwa mtu au watu kuwa huru kukutana, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine kutoa mawazo hadharani.

Mikutano ya hadhara, migomo na maandamano hayo ya amani ya CHADEMA ni sehemu ya mikusanyiko, ambayo ni haki ya kikatiba ya kila mtu au kikundi cha watu.

Mbali ya haki hiyo kuwekwa bayana kwenye Katiba ya nchi, upo utaratibu ambao umewekwa wa kuhakikisha haki hiyo inatekelezwa na wanayoitaka katika kuhakikisha wanatoa mawazo yao kupitia mikusanyiko ya aina mbalimbali.

Utaratibu ambao unavihusu vyama vya siasa mahsusi umefafanuliwa vizuri kisheria, kupitia Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992, kifungu cha 11 ambacho kinasema hivi;

“11. —(1) Every party which has been provisionally or fully registered shall be entitled-a) to hold and address public meetings in any area in the United Republic after giving notification to the police officer in-charge of the area concerned for purposes of publicizing itself and soliciting for membership;”

“…(4) When a political party is desirous of holding a meeting or procession in any open public place in any area it shall, not less than forty eight hours before the meeting, submit a written notification of its impending to the police officer in charge of the area in which the meeting is to take place is situated.

(5) The written notification referred to in subsection (4) shall specify—a) the name of the political party submitting the notification; b) the place in and time at which the meeting is to take place; c) the agenda or purpose in general of the meeting;”.

Ndugu waandishi wa habari

Vipo vifungu vingine kwenye Police and Auxiliary Service Act ambavyo navyo vinaweka utaratibu wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii, vikiwemo vyama vya siasa, kutekeleza haki hiyo, ambapo kifungu cha 43 (1) kinasema;

“Any person who is desirous of convening, collecting, forming or organizing any assembly or procession in any public place shall, not less than forty eight hours before the time when the assembly or procession is scheduled to take place, submit a written notification of his impending assembly or procession to the police officer in charge of the area specifying; (a) the place and time which the meeting is to take place, (b) the purpose in general of the meeting; and (c) such other particulars as the Minister may from time to time, by notice published in the Gazette, specify.”

Taarifa zote za CHADEMA ambazo zimetolewa kwa ajili ya mikutano, migomo na maandamano ya amani kwa Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali kwenye ngazi za majimbo, wilaya na mikoa zimezingatia wajibu wa kikatiba, matakwa ya kisheria.

Wakati watu wetu wakitimiza matakwa ya kisheria, Jeshi la Polisi kupitia barua mbalimbali, mbali ya kukiri kuwa maandamano yetu ni ya amani, limekuwa likitoa amri ambazo hazina msingi wa kisheria kuzuia mikutano na maandamano hayo. Raia mtiifu kwa nchi yake hawezi kutii amri isiyotokana na msingi wa kisheria. Kwa sababu ni batili.

Hivyo tunapenda kuwataarifu kuwa maandamano yetu ya kupinga ufisadi, uchakachuaji kwenye mchakato wa Katiba na uvunjwaji wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yako pale pale kuanzia kesho Jumatatu, Septemba 22 na kuendelea itakuwa ni wiki ya maandamano.

Ni vyema utaratibu huu tukaueleza na ueleweke vyema kwa sababu Jeshi la Polisi nchini linatumia mamlaka lisilokuwa kikatiba wala kisheria, kuzuia haki ya kikatiba ya wananchi kukusanyika na kuandamana dhidi ya jambo ambalo linafanyika kinyume na maslahi au matakwa ya wananchi.

Wanachama wetu katika maeneo mbalimbali kama ambavyo tutawaonesha kwa ushahidi hapa wa barua, wamefuata utaratibu huo wa kisheria ambao unawataka kuwasilisha barua za TAARIFA kwa Jeshi la Polisi, kuwataarifu polisi kuhusu kusudio la kufanya mkutano au kuandamana.

Tunaomba kusisitiza kuwa barua hizo ni za kutoa TAARIFA. Si kuomba KIBALI.

Pamoja na wanachama wetu katika maeneo mbalimbali ya nchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, bado wamekataliwa kutekeleza wajibu na haki yao hiyo ya kikatiba kwa kisingizio cha kunyimwa KIBALI.

Neno KIBALI, limekuwa likitumiwa na Jeshi la Polisi katika hali ile ile ya matumizi mabovu ya madaraka na mamlaka wasiyokuwa nayo kisheria wala kikatiba. Hakuna mahali popote kisheria ambapo wananchi au chama cha siasa kinatakiwa kuomba kibali ili waweze kukusanyika au kuandamana.

Jambo la pili ambalo tungependa kuzungumza hapa ni kusisitiza kuwa tunaendelea na uratibu wa maandamano ya nchi nzima, ambayo sasa tumepanga yaendelee kuanzia kesho Jumatatu.

Tunafanya hivyo kwa sababu ni wajibu na haki yetu ya kikatiba, baada ya kuwa tumefuata utaratibu wa kisheria ambao ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika. Tunapenda kuwaambia Jeshi la Polisi kuwa matumizi ya neon hilo ‘kibali’ ni ubatili kisheria na si sahihi kutii amri isiyokuwa na msingi katika sheria.

Kulaani kupigwa waandishi wa habari

Tunatumia fursa hii, kwa mara nyingine tena, kutoa kauli ya chama kulaani kwa nguvu zote kitendo cha Jeshi la Polisi kupiga waandishi wa habari waliokuwa wakitimiza wajibu wao siku ya Alhamis wakati Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe alipoitikia wito wa jeshi hilo.

Kitendo hicho cha askari wa Jeshi la Polisi kuwashushia kipigo waandishi wa habari mbele ya macho, masikio na milango ya wakubwa wa jeshi hilo na Wizara ya Mambo ya Ndani, ni wazi kimetupeleka hata nyingine katika kutaka mabadiliko makubwa ya kimfumo na kisheria kuhusu utendaji na usimamizi wa Jeshi la Polisi nchini.

Kitendo hicho kinachopaswa kulaaniwa na kila mpenda demokrasia na maendeleo, anayeamini katika uhuru wa maoni na fikra mbadala, kilitokea siku moja tu baada ya Makamu wa Rais (mkuu wa nchi kwa wakati huu) kuwa amekutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini pamoja na Vyombo vya Dola, akitoa wito kuwepo na maelewano kati ya pande hizo mbili wakati wa utekelezajiwa majukumu yao.

Tangu juzi tumemtaka Makamu wa Rais kujitokeza hadharani kuuambia umma wa Watanzania kama alitoa maelekezo mengine baada ya kuachana na wanahabari, ambayo ndiyo yaliyotekelezwa na askari siku iliyofuata!

Tumemtaka pia IGP Ernest Mangu kutoa kauli ya hatua zipi amechukua hadi sasa dhidi ya matukio mbalimbali ya askari polisi kushambulia waandishi wakiwa kazini, huku tukimkumbusha tukio la kuuwawa kikatili kwa Daudi Mwangosi katika mazingira yale yale kama ya juzi Makao Makuu ya Polisi.

Ikiwa ni sehemu ya hatua za haraka, tunawashauri vyombo vya habari nchini vikiwa kama mhimili wa nne, kuchukua hatua zifuatazo katika kuupigania mhimili huo upate hadhi na heshima unayostahili;

1. Kufuatilia na kuhakikisha kwa hatua za kinidhamu zimechukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika katika kuwashambulia na kuwapiga waandishi wa habari walipokuwa kazini wakitimiza wajibu wao.

2. Kufungua mashtaka; private prosecution kama sheria inavyoelekeza.

3. Kukusanya ushahidi wa wazi uliopo na kufungua kesi za madai, kudai fidia.

Imetolewa leo Septemba 21, 2014 na;

Kigaila Singo Benson

Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda
Add a comment...

KITENDAWILI cha iwapo wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) watarejea bungeni jana kilishindwa kuteguliwa baada ya mkutano wa mwisho wa kutafuta maridhiano kukwama.

Kikao hicho kilichoitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Francis Mutungi, kilitawaliwa na mivutano mikali baina ya wajumbe wa UKAWA na wale kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Tanzania Daima, kikao hicho kilianza kwa mkwamo baada ya wajumbe wa CCM kugoma kuanza kikao wakilenga UKAWA wasitumie umoja huo bali wajitambulishe kwa vyama vyao.

Hujuma za CCM kutaka kuwagawa wajumbe wa UKAWA zilionekana kugonga mwamba baada ya umoja huo kugomea hila hizo.

Hali hiyo ilikifanya kikao hicho kiahirishwe kwa muda kupisha majadiliano ya viongozi wakuu wa UKAWA unaoundwa na wajumbe kutoka vyama vya NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF kuteta na baadae kurejea na kukataa sharti hilo.

Kikao hicho cha jana kilikuwa ni cha mwisho kabla ya wabunge wa Bunge Maalum kuanza vikao vyake Agosti 5 mjini Dodoma.

Katika mfululizo wa vikao hivyo vya maridhiano, cha kwanza kilichofanyika wiki moja iliyopita kilimalizika bila kupatikana muafaka.

Katika kikao cha jana, inadaiwa wajumbe wanaotokana na UKAWA walipinga kwa nguvu zote mkakati huo wa kuwagawa na kueleza kwamba, walipotoka katika Bunge Maalum la Katiba, walikuwa na umoja wao na kueleza kuwa kuwatenganisha kivyama katika maridhiano hayo ni mkakati wa makusudi wa kutaka kuwagawanya ili kupenyezwe ajenda zinazowafurahisha wana CCM.

Mabishano hayo yanadaiwa kusababisha mkutano huo wa maridhiano kuahirishwa kwa muda na wajumbe kupata muda wa kupumzika kabla ya kurejea tena, huku ajenda ya kutaka kuwatenganisha UKAWA ikiwa imetupwa pembeni.

Hata hivyo, waandishi wa habari hawakuweza kupata ajenda zilizojadiliwa katika kikao na uamuzi uliofikiwa, huku Jaji Mutungi, akitaka ahojiwe yeye juu ya kilichojiri.
Hata hivyo, Jaji Mutungi, alisema kilichozungumzwa kwenye kikao hicho atakiweka wazi leo kwa waandishi wa habari.

Mbali na Jaji Mutungi, pia taarifa zinaeleza kuwa Baraza la Vyama vya Siasa, nalo litakutana kwa ajili ya kujadili yaliyojitokeza katika mkutano wa jana.

Juzi wakati wenyeviti wa vyama vinavyounda UKAWA walipozungumza na waandishi wa habari, walisema msimamo wao ni kutohudhuria vikao vya Bunge hilo kama matakwa yao hayatatimizwa.
Katika mkutano huo wa juzi, Freeman Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA, alisema wataridhia kurudi bungeni, endapo mjadala mzima utajikita kwenye rasimu ya katiba, ambayo imebeba mapendekezo ya wananchi na kutaka wajumbe wenzao, hasa kutoka CCM, kuacha kujenga hoja kwa kutumia kejeli, matusi na mizaha.

Aprili 16, mwaka huu, UKAWA walisusia vikao vya Bunge hilo la katiba, wakipinga kubadilishwa rasimu ya katiba na wajumbe wa CCM, kwa maelezo kuwa ni kinyume na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

UKAWA walidai vikao vya Bunge Maalum vilikuwa vikiendeshwa kwa ubaguzi, matusi, kejeli na kutofuata rasimu iliyowasilishwa na Tume.

source TANZANIA DAIMA .. Sauti ya Watu
Add a comment...

CHADEMA YAMSHUKIA MSAJILI.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekurupuka kutoa tamko kuhusu ukomo wa viongozi wao pasipo kuzingatia kwa ukamilifu maelezo na vielelezo vilivyopelekwa kwenye ofisi yake baada ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2006.

Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya baadhi ya vyombo vya habari kunukuu ofisi hiyo ikidai kukiandikia barua chama hicho, ambapo msajili msaidizi, Sisty Nyahoza, alisema kuwa mabadiliko yaliyofanywa katika katiba hiyo hayakufanywa na mkutano mkuu, kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa walivunja katiba.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, John Mnyika, alisema kuwa ofisi ya msajili imenukuu maelezo ya katiba ya mwaka 2004 badala ya kujikita katika katiba mpya iliyofanyiwa marekebisho makubwa na kupitishwa na mkutano mkuu wa Agosti 13 mwaka 2006.

Kwa mujibu wa Mnyika, Agosti 13 mwaka 2006, CHADEMA ilifanya marekebisho makubwa ya katiba, bendera na kadi za chama hicho na kufuta katiba ya 2004, bendera na kadi zilizokuwa zinatumika wakati huo.

Alisema ni katika mkutano huo kulifanyika mabadiliko ya kifungu cha 6.3.2 c kilichokuwa kinaweka ukomo wa uongozi, hivyo kusomeka kuwa “kiongozi anayemaliza muda wake ana haki ya kugombea tena ilimradi awe amekidhi masharti ya kuchaguliwa ambayo yameainishwa kwenye kanuni za chama kifungu cha kumi”.

Mnyika aliongeza kuwa Mbowe na Dk. Slaa bado wanazo sifa kama wakitaka kugombea kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki za chama, na kwamba wala sio kwa mujibu wa matamshi ya msajili wa vyama.

“Wenye kujua nani ana sifa ya kugombea na nani hana, maamuzi hayo hutolewa na mkutano mkuu na Baraza Kuu la chama kwa mujibu wa katiba wala hawafanyi hayo kwa maelekezo ya msajili. Msajili asubiri vikao hivyo viamue kwani ndivyo vyenye mamlaka,” alisema Mnyika.

Alimtaka msajili kufungua makabati ya ofisi yake aangalie mabadiliko yaliyofanywa na vielelezo vilivyopelekwa kwani baada ya mabadiliko hayo CHADEMA ilimwandikia msajili wa vyama wakati huo John Tedwa, ambaye alijibu kuwa alivipata na kuitambua katiba mpya iliyopitishwa na mkutano mkuu wa Agosti 13, 2006, na alihudhuria uzinduzi huo na kutoa hotuba ya kupongeza mabadiliko hayo.

Kwa mujibu wa Mnyika, suala hilo analifahamu vema kwani kwa muda huo yeye licha ya kuwa Mkurugenzi wa Vijana Taifa, pia alikuwa katibu wa kamati iliyoandika katiba mpya, baada ya kukusanya maoni ya wanachama kutoka wilayani na mikoani kuhusu marekebisho ya katiba.

“Hatua hiyo ilifuata baada ya waraka uliosambazwa nchi nzima kukusanya maoni ya wanachama, hivyo suala la marekebisho ya katiba haikuwa hoja ya Mbowe wala Dk. Slaa,” alisema.

Hata hivyo, Mnyika alitumia fursa hiyo kumuonya Msajili wa Vyama, Jaji Francis Mutungi kuwa asijivunjie heshima kama alivyofanya mtangulizi wake, kwani alianza kutumika kipropaganda hadi CHADEMA ikaamua kumsusia.

Mnyika alisema kuwa CHADEMA bado kinamheshimu Jaji Mutungi, na kwamba kuwa kauli inayonukuliwa ni ya msaidizi wake, basi msajili ajitokeze aseme kama alimtuma aseme vile alivyosema na kunukuliwa na vyombo vya habari.

“Msajili asitufikishe mahali tukaanza kumsusia, tunamwomba kama anaheshimu ofisi, aheshimu katiba za vyama, aheshimu vikao halali vya vyama, asikubali kutumika kuvuruga vyama kwa kusikiliza waasi wa vyama,” alisema.

Mnyika aliongeza kuwa CHADEMA kipo katika uchaguzi sehemu mbalimbali nchini, na kwamba hawawezi kupelekeshwa na tamko la msajili kuwataka wafanye uchaguzi kabla ya Januari kwani Kamati Kuu inayokutana Julai 18-19 mwaka huu jijini Dar es Salaam ndiyo itaamua uchaguzi mkuu ufanyike lini.

“Lakini kwa hatua tuliyofikia ya kukamilika uchaguzi wa ngazi za msingi, matawi, na kata karibu asilimia 50 nchini, uchaguzi uliobaki ni ngazi ya majimbo, wilaya na mikoa, hivyo ratiba ikiendelea vile uchaguzi wa ngazi ya taifa utafanyika Septemba mwaka huu,” alisema.

Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu, alisema msajili ajielekeze kwenye sheria na kufuata wajibu wake kwani hana mamlaka kisheria kuelekeza chama katiba iweje.

Lissu alifafanua kuwa kwa mujibu wa sheria, kazi za msajili ni kusajili vyama ambavyo katiba zao zimekidhi matakwa ya katiba
Add a comment...

Post has attachment

Add a comment...

Add a comment...
Wait while more posts are being loaded