Profile cover photo
Profile photo
Emmanuel Makwaya
118 followers
118 followers
About
Posts

Post has attachment
Add a comment...

Post has attachment
Photo
Add a comment...

Post has attachment
Add a comment...

Post has attachment

Post has attachment

Post has attachment

Post has attachment

Post has attachment
Namshukuru Mungu kwa kuniokoa nikiwa kijana. zaidi sana kunifundisha kuwa na uhusiano naye kuwa ni jambo la muhimu. nimaombi yangu kila mtu kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, sio na Mungu tu bali na watu wote wanaomzunguka.
Photo
Add a comment...

                     UHUSIANO WA MTU NA MUNGU

                                       UTANGULIZI
Uhusiano ni jambo muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Kwa sababu
hatuwezi kuishi bila kuhusiana au kushirikiana kwa namna moja ama
nyingine. Mtu huhitaji mtu mwengine ili aweze kufanikisha jambo fulani.
Mkulima anamuhitaji mwanasayansi amtengenezee mbolea mwanasayansi
anamuhiitaji mkulima ili apate chakula; daktari anamwitaji muhandisi
ili ajenge majengo na muhandisi anamuhitaji dakitari ili atibiwe hivyo
hatuwezi kukwepa mahusiano. Tunapokuwa makanisani, mchungaji
anawahitaji waimbaji ambao nao wanawahitaji waombaji, ambao nao
wanawahitaji wakarimu, watoaji, n.k. Ili kazi ya Mungu iende mbele kama
Kanisa tunahitajika kuhusiana. Paulo anasema sisi ni viungo katika mwili
wa Kristo, kama vile viungo vinavyotegemeana na kuhusiana hali kadhalika
na sisi tunapaswa kuwa hivyo.
Neno la msingi lilonifanya niandike kitabu hiki ambapo kutokea hapo
Mungu amenifundisha mambo mengi ni “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani
na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana
asipokuwa nao.” Waebrania 12:14. Hatuwezi kuwa na amani na watu wote
kama hatuna uhusiano mzuri na Mungu.

Biblia inatuonyesha mifano ya watu wengi waliokuwa na uhusiano
mzuri na Mungu jinsi walivyokuwa na amani na watu wote. Tukianza na
Yusufu mwana wa Yakobo, pamoja na kuuzwa utumwani na ndugu zake
ambao walikuwa wakimchukia, bado aliendelea kuwa na amani nao pale
walipomkuta ni kiongozi mkubwa nchini Misri (Mwanzo 37, 38, 39). Pia
tunamuona mtumishi wa Mungu Stefano katikati ya maumivu ya kupigwa
na mawe hata kufa bado na yeye alikuwa na amani na watu wale waliokuwa
wakimpiga na kuwaombea kwa Mungu asiwahesabie dhambi ile. Hata
Bwana wetu Yesu Kristo katikati ya mateso makubwa ya dhihaka na aibu,
alipongongomewa msalabani na kuchomwa mkuki ubavuni bado aliendelea
kuwa na amani na watu wote naye akawaombea kwa Baba. “Yesu akasema,
Baba uwasamehe,kwa kuwa hawajui walitendalo...” Luka 23:34.
Ni maombi yangu kwa Mungu kwamba mimi na wewe unayesoma kitabu
hiki tujifunze na zaidi sana tuwe na uhusiano mzuri na Mungu ili tuweze
kuwa na amani na watu wote pamoja na utakatifu na siku moja tumwone
Bwana Mungu mbinguni.

Kama viumbe tumeumbwa tuhusiane kwa namna moja au nyingine ili
kufanya dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi.Kama wanadamu tunahusiana na
watu, vitu, viumbe hai na visivyo hai pamoja na mazingira yanayotuzunguka.
Basi uhusiano ni kitu cha muhimu sana kujifunza.
Uhusiano ni ile hali ya vitu vyenyewe kwa vyenyewe kuwiana, hivyo basi ili
tufurahie maisha yetu ya kimwili na kiroho hatuna budi kuwa na uhusiano
mzuri. Pamoja na kwamba kuna aina mbalimbali za uhusiano kama :-
• Uhusiano wa mtu na nchi yake
• Uhusiano wa mtu na familia yake
• Uhusiano wa mtu na rafiki zake
• Uhusiano wa mtu na mchumba wake. Nk
Uhusiano wa mtu na Mungu ni ufunguo wa aina zote za mahusiano.

AINA ZA UHUSIANO
Kuna aina kuu mbili za uhusiano ambamo ndani yake mahusiano yote yapo.
1. Uhusiano mbaya
2. Uhusiano mzuri

Uhusiano mbaya
Ni ule uhusiano au hali ya kutokuwa na ushirika mzuri, maelewano mazuri
baina ya vitu vinavyohusiana. Mfano:-mwenye dhambi na Mungu, mafisadi
na nchi yao, nk

Uhusiano mzuri
Ni ule uhusiano au hali ya kuwa na ushirika mzuri, maelewano mazuri baina
ya vitu vinavyohusiana. Mfano:- Uhusiano kati ya Mungu Baba, Mungu
Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Ni wazi kwamba wengi wetu tunapenda
kuwa na mahusiano mazuri katika maisha yetu, hivyo basi vifuatavyo na
vitu muhimu katika uhusiano wa mtu na Mungu na mahusiano mengine
yeyote, upendo, msamaha, mawasiliano, uaminifu, imani, uvumilivu,
zawadi, shukurani pamoja ahadi .

Pamoja na kwamba vitu hivyo tisa juu vinawezakutufanya tuwe na
uhusiano mzuri na Mungu, bado tunahitaji kujua au kujifunza vitu vya
kuvitilia mkazo au kuwa waangalifu kwavyo ili mahusiano yetu yaendelee
kuwa mazuri. Vitu hivyo ni rafiki, ulimi na makwazo, ambapo ukijumlisha
na mambo tisa tutakuwa na mambo kumi na mbili ya kujifunza. Karibu
tunapoanza kujifunza kwa pamoja kuhusu uhusiano wa mtu na Mungu.
Naamini hutakuwa kama unavyoanza kusoma kitabu hichi.
Emmanuel Makwaya
Add a comment...
Wait while more posts are being loaded