Profile cover photo
Profile photo
MSWAHILI MCHANGA
2 followers -
Fasihi inayoeleza tamu chungu katika jamii. kiswhahili kitukuzwe

2 followers
About
Posts

Post has shared content
Ni wazi kabisa kama makalio ya mbuzi kwamba swala la utamaduni katika jamii limezua tumbo joto katika siku chache zilizopita. Ni kewli kwamba mwacha mila ni mtumwa lakini hii si sababu tosha ya kushikilia ki ki ki mila na tamaduni zilizopitwa na wakati. Kuendelea kufanya hivo na kama kujigeuza chachandu anayejipalia makaa kwa vidole vyake.

  Kwanza ni swala la ukeketaji wa ndugu zetu wa kike. Hili ni swala nyeti ambalo limepitwa na wakati. Hivi majuzi kumekuwa na tetesi kutoka kwa akina mama fulani huku juhudi zao za kushinikiza serkali iwaruhusu kutekeleza uovu huu zikigonga mwamba. Nikieleza kinagaubaga, ukweli ni kuwa shida kubwa ni kuwa wengi wa wanaoshikilia sera hii ni wale ambao hawajaelewa madhara ya vitendo hivi vya kishetani.

  Mgala muue lakini haki mpe. Jamii inakashifu ukeketaji wa vijana wa kike lakini hamna wanaume katika jamii huska wanao jitokeza kusaida kusuluhisha jambo hili.

Je, wanaume katika jamii husika watakubali kuwachumbia na kuwaoa wasichana ambao hawajapashwa tohara?

Je, jamii husika inatambua madhara ya kuwapasha wasichana tohara?

Je, wanaume wakihitajika kususia ndoa za wasichana waliopashwa tohara watakubali?

Haya ni baadhi ya maswali nyeti ambayo tunastahili kuyajibu moja kwa moja. Natoa mwaliko kwa mchango wako.

Tazama mawazo yangu kuhusu swala la mapenzi katika jamii  katika toleo langu jipya hivi karibuni

Post has attachment

Wait while more posts are being loaded