Profile

Cover photo
Haki Elimu
Attends University of Dar es Salaam
Lives in Dar es Salaam
3,567 followers|75,254 views
AboutPostsPhotosYouTube+1's
People
Have them in circles
3,567 people
Hamenya Kikoba's profile photo
Fungwa Kilozo's profile photo
Mallya Michael's profile photo
Wilfred Samwel's profile photo
Matata Mpilingondo's profile photo
Othman Abdallah's profile photo
raphael emmanuel's profile photo
wilfred mikomangwa's profile photo
Rama Mwiru's profile photo
Education
  • University of Dar es Salaam
    present
Basic Information
Gender
Decline to State
Links
YouTube
Story
Tagline
People making a difference in education and democracy
Introduction
HakiElimu is a non-profit civil society organization, founded in 2001 by a group of 13 Tanzanians who had formed a clear and longstanding commitment to transform public education for all children, having noted that education in Tanzania was in a mess, and that the many attempts to reform it had appeared to go nowhere.


Phone: +255 22 2151852/3EmailFax: +255 22 2152449Address
Physical Address Plot 739 Mathuradas Street

Bragging rights
Education
Work
Occupation
Advocacy / Activism
Places
Map of the places this user has livedMap of the places this user has livedMap of the places this user has lived
Currently
Dar es Salaam
Contact Information
Home
Phone
+255 22 2151852, +255 22 2151853
Address
Physical Address Plot 739 Mathuradas Street
Work
Phone
+255 22 2151852

Stream

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
WANANCHI WAPINGA MAAMUZI YA SERIKALI KUWABEBA WATAKAOFELI DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI : Siku moja baada ya Serikali kutangaza kuwa watakaofeli darasa la pili na kidato cha pili hawatakariri darasa bali wataendelea na madarasa ya juu huku wakichukua masomo ya ziada jioni, wadau mbalimbali wa elimu nchini wamejitokeza na kutoa maoni yao kupitia ukurasa wa kijamii unaondeshwa na shirika la HakiElimu. Wengi wamepinga uamuzi huo kwa sababu mbalimbali na kutoa angalizo kwamba kama kuna nia ya dhati ya kuboresha elimu nchini basi utaratibu wa kukariri darasa kwa waliofeli uendelee kutumika. Fungua link ifuatayo kujisomea maoni hayo http://on.fb.me/1YfRWbt
 ·  Translate
4
1
hassani Dou's profile photosimon martine's profile photoDaniel Nkuba's profile photoSekoo  Mturi's profile photo
3 comments
 
nachokiona hapa ni hali ya kukosa dira na muelekeo wa elimu yetu, naamaini TUKIJIPANGA vyema kwenye hili itatufikisha mahali pazuri. njia ya kusoma kama masomo ya ziada uku ukiendel;ea kusonga mbele si jui kama kutasaidia.
 ·  Translate
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
MATUMIZI YA KITABU KIMOJA CHA KIADA NA MTAALA WA MASOMO YA MADARASA YA CHINI. Baada ya wadau mbalimbali tukiwemo HakiElimu kupigia kelele mambo yanayorudisha nyuma elimu yetu ikiwemo mfumo wa vitabu vingi vya kufundishia na wingi wa masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili. Serikali ilitoa tamko la kurejesha mfumo wa matumizi ya kitabu kimoja cha kufundishia kwa shule zote nchini pamoja na kuanzisha mtaala mpya kwa madarasa ya chini. Je utekelezaji wa matamko hayo umefikia wapi, je watoto wa darasa la kwanza kwa sasa wanasoma masomo "kibao", je wanafunzi wote nchini wanatumia kitabu kimoja? Ungana nasi kufahamu zaidi kwa kubonyeza hapa  http://bit.ly/1Zg2lWc
 ·  Translate
5
Kifura Mukono's profile photo
 
0 
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
HAKIELIMU NA WANANCHI WAKARABATI MADARASA YA AWALI KATIKA WILAYA KUMI NCHINI. Ushirikiano kati ya Shirika lisilo la kiserikali la HakiElimu na wananchi katika wilaya kumi nchini umewezesha ukarabati wa madarasa zaidi ya 10 ya wanafunzi wa elimu awali ili kuwawezesha kupata elimu bora. Sambamba na ukarabati huo HakiElimu imewezesha ununuzi wa madawati na vifaa vya kujifunzia katika shule hizo pamoja na kuwapatia walimu mafunzo maalum ya elimu ya awali. Picha mbili hapo chini zinaonesha wanafunzi wa darasa la awali katika shule ya Msingi Ibulyu Wilayani Bariadi mkoani Simiyu waliokua wakisoma chini ya mti na hali ilivyo sasa baada ya ukarabati wa madarasa mawili katika shule hiyo.
 ·  Translate
4
1
Cosmas Joseph's profile photodaudi kelvin's profile photo
 
Hatariii sana hiio
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
WALIMU WACHARAZWA VIBOKO NA WAZAZI MWANZA
 ·  Translate
3
1
Isack Msuya's profile photodani anney's profile photo
 
Nawapa pile
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
AHADI ZA WAGOMBEA 2015
 ·  Translate
8
1
UchaguziWetu2015's profile photo
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
HONGERA kwa washindi wetu wa swali la nne la Tokomeza Zero zawadi zenu zipo njiani. Endelea kufuatilia ukurasa huu uweze kujibu swali la tano na kujishindia zawadi maridadi kutoka HakiElimu.
 ·  Translate
5
Essau George's profile photo
 
Kutowachagua wana ccm oktoba 25 ni msingi mkuu wa kutokomeza zero kwani tangu uhuru hadi leo misingi/mitaala ya elimu imezidi kushuka ikiwemo walimu kupuuzwa na kuwajali wanasiasa
 ·  Translate
Add a comment...
Have them in circles
3,567 people
Hamenya Kikoba's profile photo
Fungwa Kilozo's profile photo
Mallya Michael's profile photo
Wilfred Samwel's profile photo
Matata Mpilingondo's profile photo
Othman Abdallah's profile photo
raphael emmanuel's profile photo
wilfred mikomangwa's profile photo
Rama Mwiru's profile photo

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
WASHINDI. Hongera kwa washindi wetu wa swali la tano la Tokomeza Zero zawadi zenu zipo njiani. Endelea kufuatilia ukurasa huu uweze kujibu swali la tano na kujishindia zawadi maridadi kutoka HakiElimu.
 ·  Translate
6
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
UTEKELEZAJI WA MATUMIZI YA KITABU KIMOJA CHA KIADA NA MABORESHO YA MITAALA YA DARASA LA KWANZA LA PILI  SERIKALI JE SERIKALI IMEFIKIA WAPI?
 ·  Translate
3
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
TUNAWEZA KUJIFUNZA KITU KATIKA SHULE HIZI
 ·  Translate
3
John Lweja's profile photoCosmas Joseph's profile photo
2 comments
 
Mabadiliko muhimu
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 

Licha ya dhamira nyingi za kisiasa ambazo Tanzania imefanya kuboresha uwazi na uwajibikaji wa serikali, ripoti mbalimbali zinaonesha kwamba dhamira hizi hazijafikia viwango vya kimataifa ambavyo vingewapa wananchi haki ya kupata taarifa za umma za kibajeti ambazo zingewasaidia kuiwajibisha serikali yao.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kimataifa la International Budget Partnership (IBP), “Utafiti wa Uwazi wa Bajeti 2015” Tanzania imeshindwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa taarifa za bajeti ya taifa kwa wananchi ili kuboresha kiwango chake cha uwazi.

Baada ya kufanya tathmini kwa nchi 102 duniani, utafiti wa mwaka 2015 umebainisha kuwa Tanzania inahitaji maboresho zaidi ili iweze kutoka katika kundi la nchi zilizo katika ngazi ya kati katika Kipimo cha Uwazi wa Bajeti (OBI) ambacho hutumia vigezo vinavyokubalika kimataifa  kutoa alama za uwazi kwa kila nchi kati ya jumla ya alama 100.

Ili nchi iweze kutambuliwa kwamba inatoa taarifa kamili za kibajeti, inapaswa kupata alama zaidi ya 60 kwenye Kipimo cha Uwazi wa Bajeti.  Tanzania ilipata alama 46 kati ya 100 katika Kipimo cha Uwazi wa Bajeti, mwaka 2015, ikimaanisha kwamba serikali hutoa baadhi tu ya taarifa za bajeti kwa umma. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania huweka wazi nyaraka 6 kati ya 8 muhimu zinazopaswa kuwekwa wazi kwa umma. Hata hivyo, licha ya kuweka wazi nyaraka 6, nyaraka hizo zina baadhi tu ya taarifa ambazo haziwafanyi wananchi kuelewa ipasavyo bajeti na kuiwajibisha serikali.

Tanzania imewekwa katika kundi la nchi zilizo katika ngazi ya kati katika  Kipimo cha Uwazi wa Bajeti kwa mwaka 2015, kwa sababu serikali haitoi  taarifa za ripoti ya nusu mwaka ya utekelezaji wa bajeti na ile ya mwisho wa mwaka wa fedha kulingana na viwango vya kimataifa na imefanya vibaya katika ushiriki wa jamii na uimara wa vyombo vya usimamizi wa bajeti. Kwa mujibu wa ripoti hiyo serikali ya Tanzania imekuwa dhaifu katika kutoa fursa kwa jamii kushiriki katika mchakato wa bajeti, katika usimamizi wa bajeti kwa Bunge na ukaguzi wa bajeti wa mamlaka kuu ya ukaguzi wa bajeti  ni mdogo”

Tanzania imepata alama 33 kati ya 100 tu kwenye kigezo cha ushiriki wa wananchi katika mchakato wa bajeti. Kuhusu uimara wa vyombo vya usimamizi, Bunge lilipata alama 39 kati ya 100 na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilipata alama 50 kati ya 100 na wastani wa alama kwa upande wa uwazi wa bajeti ni 46 kati ya 100 ambayo ni alama moja tu juu ya wastani wa dunia ambao ni alama 45. Nchi ya Uganda inaongoza nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kupata alama 62 ikifuatiwa na Kenya ambayo imepata alama 48 na Rwanda imepata alama 36.
 
Kwa kuhitimisha, ripoti hiyo inasisitiza kuwa umma unahitaji kupata taarifa za bajeti na fursa ya kushiriki katika mchakato mzima wa bajeti. Hatua hii, kwa kushirikiana na usimamizi wa Bunge na vyombo vya ukaguzi wa hesabu, huchangia kuboresha uwajibikaji katika matumzi ya fedha za umma. Ushahidi unaonesha kuwa uwepo wa udhibiti katika bajeti huleta maendeleo mazuri kwa watu, hasa wale ambao ni masikini au walio katika mazingira magumu. Tanzania kukosa mwendelezo  katika kuifanya mifumo ya bajeti kuwa wazi na inayowajibika zaidi ni tatizo kubwa. Ripoti hiyo pia inapendekeza kwamba serikali inapaswa kuchuka hatua zifuatazo ili kuwa na maboresho ya haraka zaidi.

Kuboresha uwazi Tanzania inapaswa kutoa kipaumbele kwa hatua zifuatazo;
·         Kutoa ripoti ya katikati ya mwaka na ya mwisho wa mwaka
·         Kutoa maelezo ya kina zaidi kwenye Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali
·         Kutoa maelezo ya kina zaidi kwenye Bajeti iliyopitishwa
 
Kuboresha ushiriki;
Tanzania inapaswa kufanya yafuatayo kuongeza ushiriki katika bajeti
Kuanzisha mifumo ya wazi ya kupata maoni ya umma na kutoa mrejesho wa kina jinsi mawazo ya wananchi yalivyopokewa na kufanyiwa kazi.
Kuwa na vikao vya Bunge kujadili bajeti za wizara mahususi  idara na wakala mbalimbali ambapo ushuhuda toka kwa wananchi utatolewa
Kuanzisha mfumo maalumu wa ushiriki wa umma katika ukaguzi wa hesabu.
 
Kuboresha usimamizi;
Kuwa na ofisi maalumu wa utafiti wa bajeti kwa ajili ya Bunge
Kuhakikisha kwamba serikali inapata  idhini ya Bunge kabla ya kutumia bajeti ya ziada
Kupata idhini ya Bunge au Mahakama kabla ya kumuondoa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
 
Kwa ujumla, Utafiti wa Uwazi wa Bajeti wa mwaka 2015 umebaini kuwa nchi 98 kati ya 102 hazina mfumo madhubuti wa kuhakikisha kwamba fedha za umma zinatumika kwa ufanisi na kwa tija. Nchi hizo 98 zilifanya vibaya katika walau mojawapo ya vigezo vya uwajibikaji (uwazi, ushiriki wa jamii na uimara wa usimamizi); 32 kati ya nchi hizo zilifanya vibaya katika vigezo vyote vitatu. Kuongezeka kwa udhaifu wa mifumo ya uwajibikaji ni kikwazo cha utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa kama vile Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya kimataifa yanayotarajiwa kufikiwa katika Kongamano la Hali ya Hewa la Paris, mwaka 2015.

Kuhusu Utafiti wa Uwazi wa Bajeti 2015
Ripoti hii mpya inachunguza hali ya sasa ya uwazi wa bajeti na jinsi ambavyo imebadilika kulingana na muda. Ripoti inachunguza kwa kiwango gani kumekuwepo na fursa za ushiriki wa jamii katika mchako wa bajeti, na uimara wa vyombo viwili rasmi vya usimamizi, Bunge na mamlaka kuu ya ukaguzi wa hesabu. Ripoti imejikika katika Utafiti wa Uwazi wa Bajeti wa Ushirika wa Kimataifa wa Bajeti, ambao ndio kipimo huru  pekee duniani cha uwazi wa bajeti, ushiriki wa wananchi na usimamizi.  Utafiti huu hufanywa na wataalamu huru wa bajeti waliopo katika nchi zote 102 zilizofanyiwa utafiti na hupitiwa tena na wataaalamu wengine wa bajeti katika nchi husika. Serikali za nchi zilizofanyiwa utafiti hualikwa kupitia na kutoa mapendekezo kuhusu matokeo ya utafiti na kwa kiwango kikubwa nchi nyingi zimekuwa zikifanya hivyo.

Utafiti wa mwaka 2015 ni wa awamu ya tano tangu tathmini hii ya kimataifa ianze mwaka 2006.Kupata ripoti kamili na vyanzo vingine vya taarifa, ikiwa ni pamoja na matokeo ya kila nchi, tafadhali tembelea: www.openbudgetsurvey.org
 
 ·  Translate
20
2
Hussein Mdevero's profile photoyasini kiria's profile photoSudy Kazimoto's profile photoAminiel Kimo's profile photo
16 comments
 
Tanzania hakuna haki ya elimu
Mfano mdogo tu
Mtoto wa darasa la saba masomo ya darasa hawafundishwi kwa kiwango ili waingie mkakati. Sikiliza garama za mkakati kila mwezi tsh-18000 kwa miezi 8 ni sawa na tsh-144000.
Kuna haki ya elimu hapa nchini wakati mashule yamekuwa biashara kwa walimu na waratibu wa elimu. 
 ·  Translate
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
MSHINDI wa swali la nne la chemsha bongo ya Tokomeza Ziro, Ndugu Castro Beda alipotembelea ofisi ya HakiElimu kuchukua zawadi yake. Kulia ni Bi, Benedicta Mrema, Afisa Program wa Idara ya Habari na Mtangazaji wa Kipindi cha Televisheni cha Tafakari akimkabidhi Beda kifurushi cha zawadi zake. Hongera Castro Beda.
 ·  Translate
5
Rehema Mgere's profile photoHakimu Sadock's profile photo
2 comments
 
hongera sana,kwa pamoja tutaijenga elimu yetu
 ·  Translate
Add a comment...

Haki Elimu

Shared publicly  - 
 
KILA LA KHERI DARASA LA VII. Leo wanafunzi wa darasa la saba wanatarajia kuanza mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi. Tunawaombea kwa Mola wakumbuke waliyofundishwa darasani na pia wajiamini kujibu maswali kama mwanafunzi huyu anavyoonekana katika video hii .Tuna imani wanaweza na watafanikiwa. Gonga share ili kuwatakia mafanikio.
 ·  Translate
8
Vedasty Shayo's profile photo
 
Mungu awatangulie 
Add a comment...
Haki Elimu's +1's are the things they like, agree with, or want to recommend.